Uongozi wa klabu ya Dar Es Salaam Young African usiku wa December 15 tukiwa tunaelekea kufunga dirisha la usajili umetangaza kukamilisha usajili wa nyota wawili. Yanga ambao walithibitisha kumtema mchezaji wa kimataifa wa Brazil aliyekuwa anakipiga katika klabu hiyo Andry Coutinho wametangaza kusajili wachezaji wawili.
Yanga wamethibtisha kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City na baadae Mwadui FC Paul Nonga kwa mkataba wa miaka miwili sambamba na kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Niger Issoufou Boubacar kwa mkataba wa mwaka mmoja unatajwa kuwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi kama atafanya vizuri, Issoufou Boubacar ndio mrithi wa nafasi ya Andry Coutinho .
Issoufou Boubacar ambaye jana alifanyiwa vipimo vya afya na Yanga ili kukamilisha mipango ya usajili, amewahi kucheza katika klabu ya Club Africain ya Tunisia pamoja na kucheza timu yake ya taifa ya Niger kwa mechi 17 na kufunga goli mbili. Boubacar anakuwa mchezaji wa pili wa Yanga kusajiliwa kutokea Afrika Magharibi baada ya kumsajili Vincent Bossou mwanzoni mwa msimu huu kutokea Togo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.