Kama ambavyo huwa ni kawaida ya Yanga katika michezo yao ya Kimataifa huchezwa kwa kuipa majina ya Wachezaji au Viongozi wao, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe amesema Jumamosi katika mchezo dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria itakuwa ni siku ya Pacome Zouzoua “Pacome Day”.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Kamwe amesema “Tulianza na mtoko wa Max, Aziz Ki, Bacca na GSM, mchezo wetu wa awali na CR Belouizidad wengi tulifurahishwa na namna ambavyo timu ilicheza lakini tukahuzunishwa na matokeo ya mchezo”
“Mchezo huu tunakwenda na ajenda kadhaa, kushinda na kulipa deni la magoli matatu, Uongozi na benchi la fundi tumekubaliana kama Taasisi Jumamosi ikawe Pacome Day, ukisema Pacome Day mwisho unamalizia kitaalamu zaidi, unaweza kupaka rangi kichwani au kwenye ndevu, kama huwezi kupaka rangi basi unaweza kujichora chochote na Wanawake wanaweza kupaka kucha rangi”