Jumatano ya February 24 klabu ya Dar Es Salaam Young African ilikuwa mwenyeji wa klabu ya JKT Mlale katika mchezo wao wa hatua ya 16 bora yaa Kombe la FA ambalo linafahamika kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Yanga walishuka uwanja wa Taifa wakiwa wamebadili kikosi chao tofauti na kilivyozoeleka.
Kikosi cha Yanga ambacho kilisaidia kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya JKT Mlale, kiliamua kuwaanzisha wachezaji kama Matheo Anthony na Geofrey Mwashiuya na Said Juma, kwa kile ambacho kinaaminika ni kuwapumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius.
Yanga walianza kwa kuruhusu goli, baada ya Shabani Mgandila kutumia vyema makosa ya safu ya ulinzi na kupatia goli la kwanza dakika ya 22, licha ya kuwa Yanga walikuwa wanajiamini na kucheza kwa dharau, walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 38 kupitia kwa Paul Nonga na dakika ya 58 Thabani Kamusoko akapachika goli la pili na la mwisho kwa Yanga baada ya kutumia vyema pasi ya Geofrey Mwashiuya.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE