Vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu huu vinazidi kujiimarisha kwa kufanya usajili wa mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa August 6, klabu ya Dar Es Salaam Young African imemleta kiungo wa FC Platnum ya Zimbabwe Thabani Kamusoko.
Yanga imefanikiwa kumleta Kamusoko ambae amewasili jioni ya August 5 akitokea Zimbabwe na amepokelewa na meneja wa Yanga Hafidh Saleh katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) na kupelekwa moja kwa moja katika kikao na viongozi ambako kama mambo yakiwa poa atasaini mkataba wa kujiunga rasmi na Klabu hiyo.
Kamusoko anmewasili Dar Es Salaam ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka mshambuliaji wa kimataifa kutokea Liberia Kpah Sherman aondoke na kwenda kujiunga na Mpumalanga Black Aces ya Afrika ya kusini. Dirisha la Usajili litafungwa August 6 na kutakuwa na muda wa wiki moja kwa ajili ya kuwasajili wachezaji walio huru.
CHANZO CHA HII STORY>>>BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos