Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF lilianzisha sheria ya kuvitaka vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara, kulipa dola 2000 kwa kila mchezaji wa kigeni ili apate leseni. Sheria hii ilikuwa ngumu kidogo kwa vilabu kuiunga mkono, kwani dola 2000 kwa kila mchezaji ni kiasi kikubwa ukizingatia kuna baadhi ya vilabu vina miliki mchezaji wa kigeni zaidi ya mmoja.
September 11 ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kukutana na kufanya exclusive interview na katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha, ambapo klabu yao ina wachezaji wengi wa kigeni vipi kwa upande wao wamefanya maamuzi gani kuwalipia au?
“Kwa hali ya kawaida ilikuwa suala gumu kwa vilabu kukubali kulipa dola 2000, ila tumeona hata kama tukisema tunapinga, tutakosa point sasa hivi mfumo wa vilabu kwa Tanzania ni lazima ipate leseni, ili uweze kupata leseni ya klabu kuna kitu kinaitwa kiapo kutoka CAF, ambacho unapaswa kuheshimu maamuzi ya shirikisho, hivyo tumekubali kulipa licha ya kuwa hatukushirikishwa wakati sheria ikitungwa”>>> Tiboroha
Hii ni sauti ya Tiboroha
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos