Ikiwa Ligi Kuu soka Tanzania bara imesimama kupisha mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Algeria na kupisha michuano ya Kombe la Challenge hadi December 12, homa ya dirisha dogo la usajili imeanza kwa vilabu kadhaa kuanza kuhusishwa kunyemelea saini za wachezaji.
Klabu ya Dar Es Salaam Young African ilikuwa inahusishwa kutaka kusajili wachezaji wawili mmoja wa kigeni ambaye anatajwa kuja kuchukua nafasi yam brazil Andry Coutinho huku wakihusishwa kumsajili kimya kimya beki wa Simba Hassan Kessy, Amplifaya ya Clouds FM imefanya exclusive interview na katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha ana majibu haya.
” Nikwambie tu ukweli sisi tuna kikosi chetu ambacho tumekisajili toka mwanzo wa msimu kwa ajili ya mashindano tofauti tofauti ila bado sijapokea ripoti ya mwalimu akitaka kusajili, Andry Coutinho yupo na bado ana mkataba na Yanga wa miezi 8, kuendelea nae inawezekana kama mwalimu akimuhitaji, Kessy ni mchezaji mzuri na tungependa kuwa naye lakini hadi sasa ni mchezaji wa Simba wala hayupo katika mipango yetu” >>> Jonas Tiboroha
Sauti ya katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.