Mwimbaji na mtunzi maarufu wa nyimbo kutoka Nigeria Yemi Alade anasema amenusurika kwenye ajali ya gari alipokuwa akizuru nchini Uhispania.
Katika chapisho lake kwenye Instagram siku ya Jumanne, msanii huyoalifichua kuwa ajali hiyo ilitokea Alhamisi iliyopita alipokuwa akisafiri kati ya Barcelona na Benicassim.
Hakuna vifo vilivyoripotiwa.
Alisema ajali hiyo ‘ilitokea ghafla lakini alitoka akiwa na majeraha madogo, na kupoteza ukucha pekee’.
Alade, anayejulikana kwa muziki wake wa kusisimua, alisema licha ya ajali hiyo bado alitumbuiza jukwaani saa chache baadaye siku hiyo hiyo,kisha akapata ‘dharura ndogo ya matibabu’
Alimshukuru Mungu kufuatia tukio hilo akisema ‘Neema yake inatosha’.