Leo March 27, 2018 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mussa Assad amekabidhi Ripoti ya Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa Rais John Magufuli.
Kutokana na ripoti hiyo Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wawili wa halmashauri za Kigoma Ujiji na Pangani kutokana na kuwa na hati chafu za hesabu hizo, ambapo muda mfupi uliopita Waziri Jafo ametangaza rasmi kuwasimamisha kazi watendaji hao.
Ayo TV imempata diwani wa Mwanga katika Halmashauri hiyo ya Kigoma Ujiji Clayton Revocatus maarufu kama Baba Levo ambaye amefunguka kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Kigoma Ujiji.
Baba Levo ameeleza kuwa Mkurugenzi ambaye anatakiwa kujibu suala hilo ni Mkurugenzi ambaye amestaafu tangu mwezi January 2018, ambaye wamewahi kumripoti katika ofisi ya TAMISEMI kuwa atawasababishia hati chafu lakini hata hivyo hakuna hatua iliyowahi kuchukuliwa dhidi yake.
BREAKING: Waziri Jafo amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili