Mikasa siku za hivi karibuni ya Wanawake kuvamiwa na watu wasiojulikana kushambuliwa na kisha kuibiwa nywele zao nchini India inaendelea kuweka hofu tangu hali hiyo ilipoanza September 6 mwaka huu.
Inaripotiwa kuwa zaidi ya Wanawake 50 kutoka majimbo ya Haryana and Rajasthan walikumbwa na mikasa ya aina hiyo ya kushambuliwa kisha kukatwa nywele zao na baadae kukutwa wakiwa wamepoteza fahamu.
Matukio haya yameendelea kuleta hofu na kusababisha maandamano mbalimbali huku watu wakiyahusisha na masuala ya kisiasa.
India na Brazil ni miongoni mwa nchi ambazo zipo sokoni kwa muda mrefu na zinatambulika kwa kuuza nywele bandia za Wanawake ambapo rekodi zinaonyesha ndio nchi maarufu kwa kutengeneza nywele hizo ambazo nyingi pia huuzwa Afrika.
Ulipitwa na hii? MWANZO MWISHO: Tajiri Mtata alivyonunua nyumba za Bilioni 3 mnadani DSM leo
https://youtu.be/kTl6ZAZqCH0