Club ya Real Madrid ya Hispania ambao ndio Mabingwa watetetzi wa michuani ya UEFA Champions League msimu wa 2016/2017, usiku wa April 12 2017 walikuwa katika uwanja wa Alianz Arena kucheza game yao ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya FC Bayern Munich.
Real Madrid walianza kucheza game yao ya kwanza ugenini lakini licha ya kutazamiwa kukutana na ushindani mkubwa kutoka kwa wenyeji wao Bayern wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, Bayern ndio walikuwa kwanza kupata goli dakika ya 25 kupitia kwa Arturo Vidal.
Madria waliingia na plan B kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha goli na kupata goli la ushindi kupitia Cristiano Ronaldo dakika ya 47 na 77, kufunga magoli mawili leo kumemfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza kufunga jumla ya magoli 100 katika michuano ya UEFA ngazi ya club.
Cristiano Ronaldo amefunga magoli 97 katika michuano ya Champions League, magoli mawili ya UEFA Super Cup na moja katika mchezo wa UCL qualifying, kati ya magoli hayo 100 magoli 16 alifunga akiwa na Man United, michezo ya marudiano ya robo fainali ya pili itachezwa April 18 na 19.
Matokeo ya game za kwanza za robo fainali za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa April 11 na April 12 2017 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/rQ8DuAMFiS
— millard ayo (@millardayo) April 12, 2017
https://youtu.be/nt5zZ-qAdI4
VIDEO: Simba ilivyobadilisha matokeo vs Mbao FC dakika za mwisho Mwanza