Mtanzania Himid Mao kwa sasa yupo nchini Denmark kwa ajili ya majaribio yake katika timu ya Randers FC ya Denmark inayoshiriki Ligi Kuu Denmark, Himid anafanya majaribio katika timu hiyo kwa zaidi ya siku 10 lakini leo ni siku yake ya pili, katika majaribio yake pia imeripotiwa atacheza game dhidi ya AC Horsens.
1- Randers FC ni timu iliyoanzishwa January 1 2003 yaani ina miaka 14 toka kuanzishwa kwake.
2- Randers FC ni muungano wa timu sita zilizoamua kuungana na kuunda timu moja Dronningborg Boldklub (ilianzishwa 1928), Hornbæk Sportsforening (ilianzishwa 1945), Kristrup Boldklub (ilianzishwa 1908), Randers Freja (iliansihwa 1898), Randers KFUM (ilianzishwa 1920) na Vorup Frederiksberg Boldklub (ilianzishwa 1930).
3- Randers FC inayoshiriki Ligi Kuu Denmark (Danish Superligi) msimu wa 2015/2016 imefanikiwa kumaliza msimu ikiwa nafasi ya sita
4-Msimu wa 2006/2007 Randers ilifanikiwa kufuzu kucheza UEFA Cup baada ya kutwa Ubingwa wa Danish Cup, msimu wa 2009/2010 Randers walipata nafasi ya kucheza Europa League baada ya kumaliza msimu wakiwa nafasi ya pili sawa na msimu uliyofuatia wa 2010/2011.
5- Uwanja wa Randers ulijengwa mwaka 1961 na ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 18000, mwaka 1969 ukaweka rekodi ya kuchukua mashabiki 16500 katika mchezo wa UEFA Cup.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera