Kutoka Nigeria, habari ambayo imekuwa gumzo na kuzungumzwa sana ni ya mwanaume mmoja aliyeshitakiwa kwa kosa la kujifanya wakili na kufanya shughuli zote za kiwakili kwa muda wa miaka 15.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 49 alikamatwa mapema wiki hii wakati akifanya maombi ya dhamana kwaajili ya mteja wake katika mahakama ya jimbo la Lagos nchini humo.
Msemaji wa Polisi Chike Oti aliliambia Shirika la Utangazaji la BBC kuwa mtu huyo alikamatwa baada ya kushindwa kuelezea hoja yake ya kisheria pindi alipowekewa changamoto na mwanasheria mwingine aliyekuwepo mahakamani. Mtuhumiwa huyo amesema hana hatia na amepewa dhamana.
“Kama unataka kuchangisha michango shuleni lazima ufuate utaratibu” Katibu Tawala Mwakiposa
Good News kwa watumishi wote wanaoidai Serikali