Sasa ni rasmi fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 itazikutanisha timu za Real Madrid ya Hispania dhidi ya Juventus ya baada ya Real Madrid kufanikiwa kuitoa Atletico Madrid katika mchezo wa nusu fainali wakati Juventus wakiitoa Monaco.
Game ipo mapumziko Atletico 2-1 Real Madrid hili ni goli la Real Madrid limefungwa na Isco #UCL #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/q5ZHvyCyy7
— millard ayo (@millardayo) May 10, 2017
Real Madrid leo imekutana na kipigo cha magoli 2-1 katika uwanja wa Vincente Calderon kutoka kwa wenyeji wao Atletico Madrid lakini wamefuzu fainali kutokana na mchezo wa kwanza kuifunga Atletico magoli 3-0 hivyo wameitoa kwa jumla ya magoli 4-2.
Goli la pili la Atletico Madrid vs Real Madrid limefungwa na Griezmann kwa mkwaju wa penati dakika ya 16 #UCL #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/SODBVEPNMp
— millard ayo (@millardayo) May 10, 2017
Mchezo wa fainali wa UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 utachezwa katika uwanja wa Taifa wa Wales mjini Cardiff katika ya Real Madrid dhidi ya Juventus June 3 2017.
Goli la kwanza la Atletico Madrid vs Real Madrid limefungwa na Saul dakika ya 11 #UCL #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/GyHdlBqheO
— millard ayo (@millardayo) May 10, 2017
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera