Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo July 29, 2017 ametembelea Mtongani, Kunduchi ambako amekutana na wananchi wa huko na kuwahakikishia kuwa hawatahamishwa wala kubomolea nyumba zao kama ilivyoelezwa awali.
DC Hapi amewaambia wakazi hao kuwa Halmashauri ya Kinondoni imeshinda kesi ya kuwataka wananchi wa eneo hilo waondolewe lakini Serikali imesitisha mpango huo na kuwataka waishi kama kawaida.
>>>”Nyinyi ndio wapiga kura wetu. Nawahakikishia kwamba hakuna atakayekuja kuwabomolea wala kuwahamisha. Naiagiza Manispaa ianze mchakato wa kuwapimia ardhi ili shughuli za maendeleo ziendelee.” – DC Ally Hapi.
Awali, Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta alisema eneo hilo lilikuwa ni machimbo ya kokoto lakini kutokana na uharibifu wa mazingira Serikali ilifuta leseni za uchimbaji.
“Awali baada ya Serikali kushinda kesi tukafikiria tuje kuwavunjia makazi yenu lakini tukasitisha mpango huo na badala yake mtakaa hapa hapa na mtapewa viwanja vyenu kwani mpo zaidi ya 3,000.” – Benjamin Sitta.
ULIPITWA? Umoja wa Ulaya ulivyoguswa na Maendeleo Tanzania ukatoa hizi Bilioni…PLAY kwenye hii VIDEO kujua kila kitu!!!