Bado naendelea kukusogeza karibu na headlines za chaguzi ndogo zinazoendelea katika baadhi ya maeneo nchini ambapo leo Mbunge wa Muleba kusini na aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka alikuwa akimnadi mgombea udiwani katika kata ya Buhangaza iliyopo wilaya ya Muleba mkoani Kagera Jenitha Tibihenda.
Katika mazungumzo yake Prof Tibaijuka amesema…>>>”Kuna watu badala ya kujenga hoja wanapenda kufanya fujo, Serikali ya Rais Magufuli haina mchezo na niwaonye tu kwamba wagombea wote wanatakiwa kubishana kwa hoja na watu wenye kuleta vurugu hao ni watu wasio na hoja ”
“Wananchi wakifika kwenye sanduku watafanya maamuzi ingawa huwa kuna matukio yakiwemo kuwazuia watu kwenda kupiga kura huwa yanatokea haswa kwa wakinamama, CCM tupo imara na watakaoleta vurugu watatukuta tumejipanga na nikatika hali ya kuleta amani.” –Prof Anna Tibaijuka
“Nimesikitishwa na matamshi kutoka kwa Waziri” – Lowassa