Imeripotiwa kuwa club Bingwa Afrika Mashariki Azam FC ambao makao makuu yao ni Mbande Chamazi, imeripotiwa kuwa ipo katika mpango kabambe wa kuukarabati uwanja wao uwe miongoni mwa viwanja vya daraja la kwanza duniani.
Azam FC kuhakikisha kuwa lengo lao hilo linatimia wamempeleka mhandisi wao katika uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani kujifunza namna ya viwanja vinavyotunzwa, Allianz Arena kama ufahamu ndio uwanja wa nyumbani wa club ya FC Bayern Munich.
Uongozi wa Azam FC wamempeleka mhandisi wao Victor Ndonzero kuangalia miundombinu ya uwanja huo ambao ulijengwa 2006 kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia na miongoni mwa viwanja bora na vya kisasa duniani ukilinganisha na vingine vilivyojengwa miaka 100 iliyopita.
Kwa mujibu wa mtangazaji wa Azam TV Zacharia ameonesha pia FC Bayern Munich walitambua uwepo wa ugeni wa Ndonzera mhandisi wa Azam FC na kumtoa katika jarida lao kama mchezaji wao mpya, Ndonzera alitembelea Allianz Arena siku ya kuagwa kwa Bastian Schweinsteiger ambaye amestaafu soka.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe