Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji ya Mustapha Mohammed (36) Mfanyabiashara Mkazi wa Ipuli kata ya Mpela manispaa ya Tabora aliyepigwa risasi akiwa anaendesha pikipiki.
ACP Abwao amesema chanzo cha kupigwa kwake risasi wakati akiendesha pikipiki kwenda kwenye biashara zake ni ugomvi wa kibiashara ambapo Watuhumiwa na Marehemu walikuwa wakidaiana.