Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na club ya Liverpool ambapo wa sasa anaichezea Stoke City Peter Crouch, ameingia katika kitabu cha rekodi ya dunia kinachojulikana kama Guinness World Records.
Peter Crouch ambye ni mchezaji mwenye urefu wa futi 6 na inch 6, ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi ya kichwa katika Ligi Kuu England baada ya mkongwe wa zamani wa Newcastle United Alan Sheare aliyekuwa kafunga magoli 46.
Crouch anaingia katika kitabu cha Guinness World Records baada ya kufunga jumla ya magoli 53 ya kichwa, hivyo ni mchezaji aliyefunga magoli mengi ya kichwa katika historia ya EPL, Crouch amekuwa mahiri na akifunga magoli mengi ya kichwa kutokana na urefu wake.
ALL GOALS: Taifa Stars vs Malawi October 7 2017, Full Time 1-1