Siku chache baada ya Baraza la Wazee wa CHADEMA kutoa tamko kulaumu kauli ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi juu ya maoni yake kuhusu Serikali ya Awamu ya Tano, Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wasema Mzee Mwinyi hakukosea.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka amesema kauli ya Mzee Mwinyi imetokana na utendaji wa kuvutia na uchapakazi mzuri wa Rais Magufuli na ni maoni yaliyotolewa wazi bila kushurutishwa na mtu bali ni mawazo yake kama Mtanzania.
>>>“Ni ukweli usiofichika kwamba maoni ya Mzee Mwinyi bila shaka yoyote yameenda moja kwa moja kutokana na kuvutiwa na uchapakazi wa Rais Magufuli. Pia maoni hayo hayakuwa ni uwamuzi wala kushurutishwa na mtu bali ni mawazo yake kama Mtanzania na kama Mwananchi mwingine.
“Maoni ya Mzee Mwinyi yalikuwa bayana au unaweza kusema mubashara yanayoweza kumlazimisha kila binadamu mwenye akili timamu hafahamu kwa kila alichotamka katika matamshi yake. Alichokisema ni jambo lenye mantiki baada ya kuaangalia hatma ya Taifa na uzalendo wa Taifa.” – Shaka Hamdu Shaka.
VIDEO: “Nimekuteua juzi umeshaanza kufikiria Majengo, unanifanya nifikirie zaidi” – JPM