June 29, 2017 ni siku ambayo imeambatana na mambo mengi katika Siasa, Utamaduni, Jamii na Uchumi yakijadiliwa na kutolewa ufafanuzi kulingana na mahitaji na kuwasilishwa kwa njia mbalimbali zikiwemo Televisheni, Radio, Magazeti na mitandao mbalimbali.
Kama ulikosa kufahamu mambo hayo kupitia vyombo hivyo nimekukusanyia hapa na kukusogezea karibu zaidi kupitia millardayo.com.
Serikali imewataka wananchi kutunza na kulinda ujenzi wa miundombinu na kutumia fursa za uwepo wa umeme kuboresha maisha yao. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Mbunge wa Mtama @Nnauye_Nape ameitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kuzitumia Lindi na Mtwara kuingiza ktk Utalii wa Utamaduni. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Jeshi la Polisi Mwanza linamshikilia Lusato James (29) kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kaka yake anayesoma Darasa la Pili. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
"Wanasiasa ni vema wajenge fikra na kauli zenye umakini, hekina na mafunzo ya utetezi wa haki kwa kufuata sheria." – John Shibuda #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Wilaya ya Gairo, imetoa kadi 700 za Mfuko wa Bima ya Afya kwa wazee kama mkakati kuwaondolea adha wazee kupata huduma ya afya. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
"Mfanyabiashara yeyote atakayekamatwa akisafirisha mazao hayo wakati wa usiku, atachukuliwa hatua." – Anna Mghwira. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Imeelezwa kuwa 78% ya familia zina matatizo kutokana na wazazi kushindwa kutimiza majukumu yao ya malezi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Wakuu wa Mikoa na Wilaya wametakiwa kushughulikia suala la wananchi kubambikiwa kesi kwa kusimamia maadili ya watendaji wao. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa anatarajia kurejea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kujua hatma ya tuhuma zinazomkabili. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Suleiman Mathew na Ismail Kupilila wa CHADEMA baada ya kuhukumiwa miezi 8 jela. #TanzniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Polisi Tabora inawashikilia watu 41 wanaotuhumiwa kujihusisha na uganga wa jadi bila kuwa na vibali na kufanya ramli chonganishi. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa ameiagiza TANROADS kuwafukuza kazi haraka wafanyakazi wasio waadilifu ktk vituo vya mizani. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Bunge limetoa chumba maalum kwa Wabunge wenye watoto wachanga kunyonyesha watoto ikiwa ni mara ya kwanza Bunge la TZ kufanya hivyo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Watanzania wametakiwa kuacha tabia ya kubeza kazi na maamuzi mazuri yanayofanywa na Serikali badala yake waipe ushirikiano. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
TAKUKURU imesema kuwa kucheleweshwa vibali kutoka kwa DPP kunachangia baadhi ya mashauri wanayoshughulikia kutopelekwa Mahakamani. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Jeshi la Polisi Rukwa linamshikilia Japhet Kigula kwa tuhuma za kumuua mdogo wake baada ya kumpiga na mpini wa jembe kichwani. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa UDSM Salum Almas (28) unatarajiwa kuzikwa kesho ikiwa siku 50 tangu kuuawa kwa tuhuma za ujambazi. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif amesema wanatarajia kuipeleka Mahakamani RITA kwa kukiuka taratibu za sheria za chama hicho. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Maiti tatu zimeokotwa kwenye fukwe mbalimbali za Z'bar ktk siku 3 zilizopita zikiharibika kwa majeraha na kufungwa kwenye viroba. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Mauaji ya raia wasio na hatia yameendelea mkoani Pwani baada ya viongozi wawili Kibiti kuuawa kwa risasi usiku wa kuamkia jana. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Rais wa TFF, Jamal @jamalmalinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa wanashikiliwa na TAKUKURU kutokana na tuhuma za rushwa. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
TZ imeitaka Kenya kuheshimu makubaliano ya kibiashara yaliyofikiwa na Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara la A. Mashariki. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Rais JPM amekutana na Wataalamu wa umeme na ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Desalegn. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Muda wowote kuanzia wiki ijayo Tanroads itaanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zilizowekwa X ktk Barabara ya Moro kuanzia Kimara. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Halmashauri zimetakiwa kutofanya kazi kimazoea badala yake ziongeze ubunifu kuisaidia Serikali ktk kuongeza ajira kukuza uchumi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Waendesha Bodaboda wametajwa ktk utafiti kuwa wanawanyanyasa na kuwafanyia ukatili wasichana wanaokataa kushiriki nao kimapenzi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Bunge limemsimamisha Mbunge Conchesta Rwamlaza, Viti Maalum CHADEMA kutohudhuria vikao vitatu kwa kusema uongo mbele ya Bunge. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
DPP ametoa mwongozo mpya unaosisitiza kuwa hakuna dhamana kwa watuhumiwa wanaofikishwa Mahakamani kwa kesi za nyara za serikali. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
FULL VIDEO: Maalim Seif aituhumu Taasisi ya Serikali, Msajili!!!