Mchezaji kinda wa kitanzania Rabbin Sanga kutoka kituo cha soka cha Bom Bom SC amefanikiwa kuanza salama majaribio yake ya siku 10 katika kikosi cha timu ya vijana ya Besiktas ya Uturuki, Rabbin ameanza mazoezi jioni ya leo na wachezaji wenzake ambapo ushirikiano ulikuwa mkubwa.
Rabbin Sanga aliyeambatana na mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffid Dauda, alipata nafasi hiyo ya kwenda kufanya majaribio Besiktas baada ya kuibuka mchezaji bora wa michuano ya Ndondo Cup Academy iliyokuwa inahusisha vijana wenye umri chini ya miaka 16.
Michuano ya Ndondo Cup mwaka jana ilikuwa inadhaminiwa na kampuni ya beko ambao ni wadhamini wakuu wa club ya Besiktas hivyo waliahidi mchezaji bora wa michuano hiyo kupewa zawadi ya kufanya majaribio katika club ya Besiktas na kama atafuzu basi atasalia katika timu hiyo.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF