Licha Serikali kupiga hatua kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kiafya kwa kwa ukaribu lakini Bado wananchi katika Kijiji cha Nyarutefye Kata ya Buziku Halmashauri ya wilaya ya Chato Mkoani Geita Bado wanakumbana na changamoto ya kufuata huduma ya kituo cha Afya kwa zaidi ya 20km hali ambayo inawafanya watoa huduma kuja Mara mbili kwa mwezi ili kutoa huduma za kliniki.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyarutefye Bi. Beliana Manumbu wakati akisoma Taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Zahanati ya kijiji mbele ya Kamati ya siasa ya wilaya ya Chato ambayo imetembelea Miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa Zahanati hiyo ambayo haijakamilika kwa kipindi cha Miaka 12 kutoka Mwaka 2009.
” Kijiji cha Nyarutefye kilianza ujenzi wa zahanati ya kijiji Mnamo mwaka 2009 kwa michango ya nguvu ya wananchi kwa ramani iliyotolewa na Halmashauri na ilipofika mwaka 2012 Boma lilikamirika kwa thamani ya shilingi Milioni 15.80 fedha zote hizo ni michango ya wananchi , ” Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyarutefye , Beliana Manumbu.
Barnabas Nyerembe ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Chato amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ya Chato aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato kuja na Majibu ya kukamilisha Boma la Zahanati hiyo ndani ya siku tatu ambayo limekuwa changamoto kukamilika.