Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashimu Komba amesikitishwa na kitendo cha ujenzi wa Zahanati iliyopo Kata ya Kasamwa Wilayani humo kutokukamilika toka mwaka mwaka 2019 huku hadi sasa shilingi milioni 100 zikiwa zimeshatumika kwenye ujenzi wake.
Akiwa katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kasamwa, DC Komba amesema toka ameripoti kazini kupitia taarifa mbalimbali ambazo amekuwa akipokea kupitia CSR, miradi hiyo imekuwa haikamiliki kwa wakati ambapo imembidi kuagiza upya kukamilisha kwa miradi yote ya CSR ikiwemo Zahanati hiyo.
“Toka niliporipoti sikufurahishwa sana na kukutana na hoja ya miradi ya CSR kutokamilika, Wananchi hawa wanataka maendeleo Zahanati ya milioni 100 imeanza kujengwa 2019 haijakamilika, 2020 haijakamilika, 2021 haijakamilika 2022 haijakamilika, 2023 leo tuko mwaka wa 2024 tunapokuwa na miradi mingi haijakamilika tunawafanya Wananchi hawa wasione kama kuna Faida” ——— DC. Komba.