Zaidi ya watu 2,400 waliuawa nchini Haiti tangu kuanza kwa 2023 huku kukiwa na kukithiri kwa ghasia za magenge, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 350 waliouawa kwa kushambuliwa na wenyeji na makundi ya wapiganaji, Umoja wa Mataifa ulisema Ijumaa.
“Kati ya Januari 1 na Agosti 15 mwaka huu, watu wasiopungua 2,439 wameuawa na wengine 902 kujeruhiwa,” msemaji wa ofisi ya haki za Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.
Takriban watu 3,120 wamekimbia wilaya hiyo, kulingana na makadirio ya Idara ya Ulinzi ya Raia ya Haiti na maafisa wanasema kuna uwezekano mkubwa kufuata.
Kitongoji hicho hushambuliwa mara kwa mara na genge linaloongozwa na Renel Destina, anayejulikana kwa jina la Ti Lapli, ambaye anatafutwa na mamlaka ya Marekani kwa kuwateka nyara raia wa Marekani.
“Maafisa wa polisi wanaoishi eneo hilo hawana tena mbinu za kututetea, matokeo yake majambazi hao waliweza kuchukua makazi yetu,” alisema Derisca.
Aliongeza kuwa wahalifu walipora na kuchoma moto nyumba za mtaa huo na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
Mamlaka ya Haiti pia ilisema kuwa nyumba katika eneo hilo zimeteketezwa na kwamba kumekuwa na “hasara ya maisha ya binadamu”, lakini hawakutoa maelezo maalum.