Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema kuwa zaidi ya asilimia 90 ya waajiriwa katika kampuni za gesi asilia zilizopo hapa nchini ni watanzania.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa kitengo cha ushirikishwaji Wazawa na Uhusishaji wa Wadau kutoka Pura, Charles Nyangi wakati akizungumza na waandiahi wa habari katika maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba.
Nyangi amesema aslimia 60 ya watoa huduma, wasambazaji wa bidhaa hizo za Gesi asili na malighafi ni watanzania pia na asilimia 40 ikiwa ni kampuni mbalimbali kutoka nje ya nchi.Amesema ushiriki wa watanzania umeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma na kwamba Pura kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti na Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa kazindata ya kusaidia wataalam mbalimbali wa masuala ya mafuta na gesi kupata ajira kwa urahisi zaidi.
“Kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana tumeanzisha kazindata kwa kushirikiana na EWURA kuandaa wataalamu na kuwatambua kiurahisi pindi ajira zinapopatikana,”amesema na kuongeza
“Kazindata hii imeanza kutumika tangu mwezi Mei mwaka huu, tumeanza kuandikisha kupitia website yetu na fomu maalum ambazo wanajaza,miaka ya nyuma watanzania walikuwa wanapoteza fursa,”amesema
Aidha amesema wapo katika maonesho haya ya Sabasaba ya 46 kwa lengo la kutoa elimu juu ya kazi wanazofanya ili wananchi waweze kuzitambua na kuzijua katika utafutaji,uchumbaji nabusambazaji wa Gesi na Petroli.
Nyangi amesema wanaendelea kutoa wito kwa jamii kujitoleza kwa wingi katika banda lao kujifunza na kuona fursa mbalimbali zinazopatikana katika taasisi yao ambayo ni mpya.
“Tunawajengea uelewa wananchi kupitia makongamano mbalimbali kama haya katika kupata fursa mbalimbali za Mafuta na Gesi asilia zilizopo nchini,” amesema