Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego amesema mkoa wa Iringa umepokea zaidi ya bilioni 100 kwaajili ya ubereshwaji wa huduma za upatikanaji wa maji vijijini
Halima Dendego ameyabainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwenye mkutano ulioandaliwa na idara ya maelezo ambapo amesema kutokana na adha wanayokumbana nayo wanannchi waishio vijijini ya ukosefu wa maji serikali ya awamu ya sita yenye lengo la kumtua mama ndoo kichwani imetoa fedha nyingi zitakazokwenda kusaidia tatizo hilo
Pia Dendego amesema pamoja na mabilioni ya kuboresha huduma za maji serikali imetoa shilingi bilioni 68 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya elimu na msingi na sekondari kwenye halmashauri tano za mkoa.
Vilevile Kastori Msigala mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ametaja mafanikio katika sekta ya Afya katika manispaa ya Iringa ikiwemo hospitali kwasabbau mwanzo kulikuwa hakuna hospitali ila sasa ipo hospitali kubwa ya Frelimo na kwenye hospitali hiyo kunayo majengo mazuri ikiwemo pia jengo la mama na mtoto
“ Kuna majengo ambayo yanatumika kama wodi ya wanawake na wanaume na tumepata miundombinu ya majenereta na miundombinu ya kuhifadhia maiti kwahiyo kwa kipindi kifupi tumefanikiwa sana”
“ Nichukue nafasi hii kumshukuru Rais kwa kutoa fedha nyingi na niombe asituchoke aendelee na sisi tujitahidi kwa namna tutakavyoweza ili kuweza kutekeleza mambo mbalimbali na kusaidia wanannchi wetu “ amesema Kastori Msigala Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa