Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) imekamata zaidi ya kilo 1 ya dawa ya methamphetamine yenye thamani ya Shilingi milioni 9m.
Kulingana na DCI, dawa hizo zilizonaswa siku ya Jumanne zilikuwa zimefichwa ndani ya tandiko za baiskeli na zilikuwa zikielekea mjini Jakarta, Indonesia.
Walisema shehena hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Moroni, Comoro.
“Wapelelezi waliotumwa katika uwanja wa ndege kukabiliana na uhalifu wa uhamiaji na mizigo inayotiliwa shaka ilikuwa imekusanyika katika kibanda cha DHL kwa ajili ya zoezi la uhakiki, ambapo vifurushi vya rangi ya kahawia vilipatikana vimefichwa kwenye viti vya baiskeli kumi na moja,” DCI ilisema.
Vipimo vilithibitisha kuwepo kwa dawa aina ya methamphetamine.
DCI ilisema operesheni za interpol zimeanzishwa kutafuta wahusika ili wakamatwe na kufunguliwa mashtaka