Mkurugenzi wa Kampuni ya nguzo za umeme Nchini (Qwihaya Company Enterprises) Leonard Mahenda amemshuruku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaamini wawekezaji wazawa na kuwapa kipaumbele katika sekta ya uwekezaji hapa nchini.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 17 tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho,,Mahenda amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji,hali iliyo muwezesha kufungua Viwanda vingine vya kuchakata nguzo za umeme katika mkoa Pwani- Kibaha,Njombe na Kigoma.
Mahenda alisema kwa asilimia 49 ya wawekezaji nchini ni wazawa,hali iliyochangia na Serikali nzuri iliyopo madarakani kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji hasa kwenye kipengele Cha mitaji.
Aidha ametaja moja ya mafanikio aliyoyapata katika kipindi Cha miaka mitatu ya Rais Samia kuwa ni kufungua Viwanda vingine pamoja na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 300 ambao asilimia kubwa ni wazawa wa maeneo husika.
Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 katika kusherekea siku ya kuanzishwa leo February 12/2024 imewatembelea na kuwapa mkono wa pole ikiwemo kukabidhi vifaa mbali mbali kwa wagonjwa wote waliolazwa katika Hospitali ya mji wa Mafinga,wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
Hatahivyo kampuni hiyo imetoa misaada wa vitu mbali mbali kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu kwenye hospitali ya mafinga mji ikiwa ni kuthamini mchango wa jamii katika kukuza sekta ya viwanda nchini.