Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elika amezindua ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa wananchi wa wilaya za Nyamagana na Ilemela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Balandya amebainisha kuwa tayari NIDA imekamilisha uzalishaji wa Vitambulisho kwa wananchi wapatao 716, 245 na kwamba vingi bado vipo kwenye Ofisi za Serikali za Mitaa, huku wananchi wakiwa na namba tu za kuwatambua jambo ambalo si sahihi hivyo ni wakati sasa wa kupatiwa kwa ajili ya rejea mbalimbali.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mwanza Daud Abdallah ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwani kigezo kikubwa cha utambuzi na usajili ni kwa raia kuwa na umri 18 na kwamba Mamlaka hiyo imesajili asilimia 84 ya wenye sifa mkoani Mwanza huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.