Zaidi ya wananchi elfu 16 wa kata ya Gehandu Wilaya ya Hanang wameanza kunufaika na mradi mkubwa wa maji wa Mogitu-Gehandu unaotekelezwa na serikali kwa zaidi ya shilingi bil 6 ambapo mradi huo utaondoa adha ya miaka tangu kupatikana kwa uhuru ya wananchi kufuata huduma ya maji umbali mrefu kwa saa 16.
Kutokana na utekelezaji wa mradi huu wananchi wa kata ya mogitu wakizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Manyara kutembelea miradi ya maji na sekta nyingine ikiwemo afya wametoa shukrani zao kwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi aliyoitoa mwaka 2020 wakati kampeni akiwa makamu wa rais katika serikali ya awamu ya tano.
Meneja wa Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Wilaya ya Hanang Mhandisi Hubert Kijazi amesema mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 96 ukijumuisha vituo 50 vya kuchotea maji
Nae Mkuu mkoa Sendiga katika ziara yake hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maji wilayani amewataka wananchi kuitunza miradi hiyo ambayo Serikali imetumia gharama kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
Queens Sendiga pia ametembelea mradi mwingine wa Ruwasa unaotekelezwa kwa shil mil 300 uliopo kijiji lalaji unaotarajiwa kuhudumia wananchi zaodi ya 2000.