Zaidi ya Wapalestina 1,300 sasa wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel, Gaza imesema, huku vifaa katika Ukanda huo unaozingirwa vikisalia kukatika.
Wizara ya Afya ya Gaza ilisema kuongezeka kwa vifo vya Wapalestina sasa ni 1,354, na kwamba wengine 6,049 wamejeruhiwa tangu Jumamosi.
Wakati huo huo, serikali ya Israel imesema hakutakuwa na umeme, mafuta au maji kwa wale walio katika Ukanda huo uliofungwa hadi mateka wake wote waachiliwe.
“Msaada wa kibinadamu kwa Gaza? Hakuna swichi ya umeme itainuliwa, hakuna bomba la maji litakalofunguliwa na hakuna lori la mafuta litakaloingia hadi mateka wa Israeli warudishwe nyumbani,” Waziri wa Nishati wa Israeli Israel Katz aliandika kwenye X siku ya Alhamisi.
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu “janga la kibinadamu” linalotokea katika eneo hilo, wakati Shirika la Msalaba Mwekundu limeomba mafuta yaruhusiwe ili kuzuia hospitali zilizozidiwa “kugeuka kuwa vyumba vya kuhifadhia maiti”.
Haya yanajiri wakati mamia kwa maelfu ya wanajeshi wa Israel (IDF) wamekusanyika kwenye mpaka wa eneo hilo, wakiwa tayari kuivamia Gaza, huku msemaji wa jeshi la Israel akisema siku ya Alhamisi “wanajiandaa kwa manuva ya ardhini iwapo itaamuliwa” .
Wanamgambo wa Gaza wanawashikilia takriban watu 150 waliochukuliwa mateka kutoka Israel. Jeshi la Israel limesema zaidi ya watu 1,200 wameuawa nchini Israel.