Zaidi ya Wapalestina 35,562 wameuawa na 79,652 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza tangu Oktoba 7, wizara ya afya katika eneo lililozingirwa imesema.
Wizara hiyo ilisema kuwa watu 106 waliuawa na 176 kujeruhiwa katika kipindi cha hivi punde cha kuripoti cha saa 24, kulingana na Al Jazeera.
Idadi ya waliofariki inakadiriwa kuwa kubwa zaidi huku maelfu wakiaminika kufukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka wakati wa mashambulizi ya Israel.
Israel iliendesha vita vya mauaji ya halaiki katika eneo la Ghaza lililozingirwa tarehe 7 Oktoba baada ya kundi la Muqawama la Hamas la Palestina kutekeleza operesheni ya kihistoria dhidi ya utawala huo ghasibu kwa kulipiza kisasi dhulma zinazozidi kufanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Palestina.
Israel imeweka mzingiro kamili katika eneo hilo lenye watu wengi, na kukata mafuta, umeme, chakula na maji kwa Wapalestina zaidi ya milioni mbili wanaoishi huko.