Baada ya takriban siku 100 za vita huko Gaza, zaidi ya watoto 10,000 – au 1% ya jumla ya watoto wote wa Ukanda wa Gaza – wameuawa, kulingana na ripoti mpya kutoka shirika ka Save The Children. Watoto walionusurika vitani “huvumilia mambo ya kutisha yasiyoweza kuelezeka, hususan majeraha yanayobadilisha maisha, kuchomwa moto, magonjwa, kutopata matibabu ya kutosha, na kufiwa na wazazi wao na wapendwa wengine,” ripoti hiyo imesema.
Kati ya maelfu ya watoto waliojeruhiwa, angalau 1,000 walipoteza mguu mmoja au yote miwili, kulingana na ripoti hiyo. Kila siku tangu kuanza kwa vita hivyo, zaidi ya watoto kumi wamepoteza angalau mguu mmoja au yote miwili, wengi walikatwa viungo hivyo bila kupigwa ganzi.
“Idadi hiyo sio tu ya kushangaza katika ukubwa na upeo wao, lakini pia katika athari zao halisi,” Jason Lee kutoka shirika hilo lisilo la kiserikali la ameiambia Al Jazeera. “Sio takwimu tu. Kila mmoja wao ni mtoto.”