Zaidi ya watoto laki nne wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Polio Mkoani Manyara kwaajili ya kuwakinga na ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha maradhi mbalimbali ikiwemo ulemavu pamoja na Vifo.
Afisa afya mkoa wa Manyara Sultan Mwabulambo amesema zoezi hilo litaanza December 1 hadi 4 mwaka huu ambapo wataalamu watapita nyumba kwa nyumba,mashuleni na katika maeneo yenye mikusanyiko ili kuwafikia watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Nae mratibu wa chanjo mkoa wa Manyara Seleman Manoza amesema chanjo hiyo ni muhimu kwa watoto ili kuwanusuru na magonjwa mbalimbali hivyo wazazi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya pindi wanapofika katika maeneo yao.
Amesema watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano wapi kwenye hatari zaidi ya ugonjwa huo kutokana na mazingira ya ukuaji wao tofauti na watoto wa miaka mitano na kuendelea.