Takriban watu 107 walikandamizwa hadi kufa katika mkutano wa kidini wa Kihindu kaskazini mwa India siku ya Jumanne, na wengine wengi kujeruhiwa, afisa mkuu wa serikali alisema.
Umati mkubwa ulikuwa umekusanyika karibu na mji wa Hathras kwa ajili ya mahubiri ya mhubiri maarufu lakini dhoruba kali ya vumbi ilizua hofu watu walipokuwa wakiondoka.
Wengi walikandamizwa au kukanyagwa, wakianguka juu ya kila mmoja, huku wengine wakianguka kwenye mfereji wa maji kando ya barabara katika machafuko hayo.
“Waliohudhuria walikuwa wakitoka nje ya ukumbi wakati dhoruba ya vumbi ilipofusha macho yao, na kusababisha ghasia na tukio la kusikitisha,” alisema Chaitra V., kamishna wa tarafa ya mji wa Aligarh katika jimbo la Uttar Pradesh, aliiambia AFP.