Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo alitangaza kuwa watu 304 walikamatwa wakati wa operesheni ya “shujaa-34” katika miji 32.
Polisi wa Uturuki wamewakamata zaidi ya watu 300 kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo wa Islamic State (ISIS) wakati wa msako mkali katika miji 32, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ametangaza.
“Watu 304 walikamatwa wakati wa operesheni ya “shujaa-34” iliyofanywa wakati huo huo katika miji 32 dhidi ya kundi la kigaidi la “Daesh”, Ali Yerlikaya aliandika kwenye X – zamani Twitter.
‘Daesh’ inarejelea kifupi cha Kiarabu cha shirika la Islamic State.
Istanbul na mji mkuu, Ankara, ni miongoni mwa maeneo 32 ambapo operesheni ya polisi ilifanywa.
Takriban watu 86 walikamatwa katika jiji la Istanbul pekee, Yerlikaya alisema.
Uturuki ilikuwa eneo la mashambulizi mengi kati ya 2015 na 2017 – ambayo baadhi yalihusishwa na Islamic State.