Shule nchini Zambia zimefunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu baada ya kucheleweshwa kwa mara kadhaa kutokana na mlipuko wa kipindupindu.
Siku rasimi ya kufunguliwa kwa shule ilichelewesha kwa wiki tano kama sehemu ya hatua zilizochukuliwa kudhibiti msambao wa ugonjwa huo hatari.
Wizara ya elimu kwenye taifa hilo imesema itafanya uchunguzi wa kina kutathmini namana shule zilivyojianda kwa ajili ya ufunguzi.
Hatua hii imekuja wakati huu mamlaka kwenye taifa hilo ikieleza kuwa msambao wa kipindupindu umeanza kupungua.
Karibia watu 500 wameripotiwa kufariki tangu mlipuko huo kuthibitishwa mwezi Oktoba mwaka uliopita.