Leo September 8, 2018 Serikali ya Zambia ipo kwenye mazungumzo na China ili kuangalia uwezekano wa kuwapa Shirika la Umeme la nchi hiyo (ZEWASCO) hii ni baada ya kushindwa kulipa deni kubwa wanalodaiwa na Serikali hiyo.
Taasisi ya Kimataifa ya Fedha (IMF) imepata wasiwasi kuwa huenda China ina mkakati wa kutoa mikopo isiyolipika ili wataifishe rasilimali za wadeni wawanao wadai.
China imeonekana kuwa nchi rafiki kwa Mataifa ya bara la Afrika lakini inatabiriwa kuwa siku moja itayazika Mataifa hayo katika dimbwi la madeni makubwa.
Rasilimali za nchi zitakazoshindwa kulipa madeni zitataifishwa na uhuru wa kujiamulia mambo wa nchi utakuwa mashakani.