Habari ya Asubuhi na karibu kwenye matangazo yetu mubashara hii leo…
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza mnamo Agosti 11 kuwafuta kazi maafisa wote wa kikanda wanaohusika na kuajiri wanajeshi wapya ili kukomesha mfumo wa rushwa unaowaruhusu askari kutoroka jeshi na kumtaja Roustem Oumerov waziri mpya wa ulinzi wa nchi hiyo.
Roustem Oumerov atakuwa Waziri mpya wa Ulinzi, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza Jumapili usiku. Anachukua nafasi ya Oleksiï Reznikov. Roustem Umerov ni kiongozi mashuhuri wa jumuiya ya Kitatari ya Crimea ambaye aliwakilisha Kyiv katika mazungumzo nyeti na Moscow.
Bw. Umerov, 41, alizaliwa katika jamhuri ya zamani ya Soviet ya Uzbekistan, ambapo familia yake ilikimbilia uhamishoni chini ya utawala wa Stalin, na alikuwa mtoto wakati familia yake ilipohamia Crimea wakati Watatari waliruhusiwa kurudi, katika miaka ya 80 na miaka ya 90. Alianzia katika tasnia ya mawasiliano mnamo 2004, na ni mbunge tangu mwaka 2019.
Katika Bunge, alikuwa mwenyekiti mwenza wa Jukwaa la Crimea, ambalo liliratibu juhudi za kidiplomasia za kimataifa za kufuta hatua ya Urusi ya unyakuzi wajimbo hilo la Crimea mwaka 2014. Kwa miaka mingi alikuwa mshauri wa kiongozi wa kihistoria wa Tatari ya Crimea, Mustafa Dzhemilev.
Urusi iliidhinisha unyakuzi wake wa Crimea kwa kura ya maoni iliyochukuliwa kuwa kinyume cha sheria na Ukraine na washirika wake wa Magharibi. Watatari, ambao wanajumuisha 12% hadi 15% ya wakazi wa Crimea, kwa kiasi kikubwa walisusia kura hii ya maoni. Kwa sababu hiyo, Moscow iliharamisha Mejlis, kusanyiko la kitamaduni la Waislamu wachache wa Kitatari, na kulitaja kuwa kundi lenye msimamo mkali, ambalo wanachama wengi walifungwa gerezani.