Rais wa Marekani Joe Biden amemwalika mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mkutano katika Ikulu ya Marekani, siku ya Jumanne (Des 12) huku kukiwa na mkwamo katika Bunge la Marekani kuhusu msaada kwa Ukraine.
Rais wa Ukraine amealikwa kuhutubia Maseneta wa Marekani siku ya Jumanne (Desemba 12) katika ikulu ya Capitol, msaidizi wa uongozi wa Seneti alisema Jumapili (Desemba 10).
Zelensky pia atafanya mkutano wa faragha na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Mike Johnson Jumanne, alisema msemaji wa Johnson Raj Shah katika barua pepe kwa Reuters.
Ziara ya rais wa Ukraine mjini Washington pia itajumuisha ushirikiano wa kiulinzi kati ya Washington na Kyiv “hasa kupitia miradi ya pamoja ya utengenezaji wa silaha na mifumo ya ulinzi wa anga, pamoja na uratibu wa juhudi kati ya nchi zetu katika
Wiki iliyopita, maseneta wa Republican walizuia msaada wa dharura wa dola bilioni 106 hasa kwa Ukraine na Israel wakitaja kutokuwepo kwa mageuzi ya uhamiaji waliyodai kama sehemu ya kifurushi hicho.
Hata hivyo, hawaonekani kuwa karibu na mpango unaounganisha mabadiliko ya sera ya uhamiaji na mpaka kwenye kifurushi cha msaada wa dharura.