Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepanga kumsajili nyota wa Liverpool, Mohamed Salah katika dirisha la usajili la msimu ujao, baada ya ligi mbalimbali kumalika mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka huu.
Nyota huyo wa Liverpool amekuwa akihusishwa kuondoka katika klabu hiyo kutokana na kutoa kauli tata siku za hivi karibuni kuwa “Madrid na Barcelona ni timu bora” amewahi kusema Salah.
Salah 28, raia wa Misri katika mechi tatu zilizopita hajatupia kambani bao, jambo lililoibua maneno kutoka kwa mashabiki juu ya uaminifu wake kwa klabu.