Mwaka 2006 staa wa soka wa kimataifa wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria Zinedine Zidane aliingia katika headlines wakati wa mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2006 katika mchezo dhidi ya Italia, Zidane aliingia katika headlines baada ya kumpiga kichwa Marco Materazzi kutokana na kutolewa kauli ambayo hakuipenda.
Kuna msemo unasema like father like son, mtoto wa staa huyo anayeichezea timu ya vijana wenye umri chini 17 ya Real Madrid Luca Zidane ameingia katika headlines za baba yake baada ya kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid kwa tukio kama alilofanya baba yake, mchezo ambao ulimalizika kwa Real Madrid kufungwa goli 4-2.
Zidane ana watoto wanne ambao wote wanacheza soka Enzo (20) ndio mkubwa yupo Real Madrid Castilla, Theo, Elyaz pamoja na Luca ambaye anacheza nafasi ya golikipa na ndio aliyofanya tukio kama la baba yake.
Video ya tukio la Zinedine Zidane la kumpiga kichwa Marco Materazzi 2006.
Video ya tukio la mtoto wake Luca
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.