Kwa kipindi cha Miaka 19 mfululizo miongoni mwa matamasha makubwa yanayokusanya watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti Duniani ni pamoja na tamasha la Zanzibar International Film Festival ‘ZIFF’ ambalo hili limejikita zaidi kwenye upande wa filamu.
Isiaka Mlawa ambaye ni Meneja Masoko wa ZIFF amesema mwaka 2016 umekua tofauti kwao kwa sababu wamepokea zaidi ya filamu 400 kutoka nchi tofauti na baada ya kupitiwa na kuchujwa ni filamu 90 tu ndizo zimepita kwa kukidhi vigezo vyao .
Ndani ya filamu 90 zilizopita,kwa mara ya kwanza Tanzania tumepitisha filamu 16 ambapo Tanzania bara zikiwa 12 na Tanzania visiwani(Zanzibar) filamu 4,Mlawa amesema Watanzania wengi wamekua na hofu ya kuhudhuria matamasha kama haya kwa kuhofia viingilio na kusema kuwa kiingilio kikubwa cha ZIFF ni Tsh.5,000 na amesema kuangalia filamu ambayo kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku hakuna malipo yoyote ni bure,malipo yanahusu zaidi utumbuizaji (performance) na shughuli ya utoaji wa tuzo.
Nimekurekodia pia video mtu wangu unaweza kubonyeza play hapo chini kutazama.