Wizara ya Afya leo December 16 2016 imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania.
Taarifa imesema kama ilivyosema wizara mwezi February 2016, ugonjwa wa ZIKA bado haujaingia Tanzania na anawatoa hofu Wananchi kuwa kwa sasa Tanzania ugonjwa huo haujathibitishwa kuwepo.
Wizara imesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya utafiti (NIMR) ulikuwa ni utafiti uliofanywa kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupimia magonjwa ya ZIKA na CHIKUNGUNYA lakini kwa taratibu wa kitafiti, hii ni hatua ya awali ya kuangalia ubora na uwezo wa kipimo hicho.
Tazama video hii fupi hapa chini anayoongea Naibu Waziri wa Afya Dr. Kigwangalla.
Wizara ya Afya imewatoa hofu Watanzania kuhusu taarifa za virusi vya ugonjwa wa ZIKA, Waziri @UMwalimu na naibu @HKigwangalla wafafanua leo. pic.twitter.com/y3VGcmabjd
— millard ayo (@millardayo) December 16, 2016
VIDEO: Majibu ya serikali kuhusu wanaosubiri ajira za Ualimu, tazama hii video hapa chini
VIDEO: Tazama Makomandoo wa Tanzania walivyoonyesha uwezo mbele ya Rais Magufuli… kwenye hii video hapa chini