Mamlaka nchini Zimbabwe imetangaza hali ya dharura kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika mji mkuu wa Harare.
Tayari watu kadhaa wameripotiwa kufariki kutokana na maradhi yao wakati zaidi ya watu wengine elfu saba wakithibitishwa kuambukizwa.
Mamlaka ya jiji inasema msambao wa maambukizi hao kwenye jiji hilo, unatoa kumbukumbu ya kilichotokea mwaka mwa 2008 ambapo maelfu ya watu walifariki baada ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Meya wa jiji hilo la Harare, Ian Makone, akizungumza na vyombo vya habari vya ndani amethibitisha kutangazwa jwa hali hiyo ya dharura.
Uongozi wa jiji sasa unatoa wito wa kuungwa mkono kuzuia kasi ya msambao wa maradhi hayo ikiwemo upatikanaji wa maji safi.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu (IFRC), mamlaka ya jiji imekuwa ikikabiliwa na wakati mgumu kutoa huduma kwa idadi kubwa ya wagonjwa kutokana na mlipuko huo.