Serikali ya Zimbabwe imetangaza mikakati ya kudhibiti mlipuko wa kipindupindu ambao umedaiwa kuua zaidi ya watu 100.
Mikakati hiyo ni pamoja na kuzuia baadhi ya mikusanyiko ya kijamii na kudhibiti idadi ya watu wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi katika maeneo yaliyoathiriwa na mlipuko huo.
Wilaya kadhaa na mji mkuu Harare, zimeripotiwa kuathirika na mlipuko huo.Utoaji wa chakula kwenye mazishi pia kumepigwa marufuku.
Wizara ya afya siku ya Jumatano, ilitangaza kutokea kwa vifo 100 vinavyohusishwa na kipindupindu, 30 kati ya waliofariki wakithibitishwa kufariki baada ya kuambukizwa virusi hivyo.
Wizara hiyo pia ilithibitisha visa 905 vya kipindupindu kati ya visa zaidi ya 4,600 vinavyoshukiwa kuwa ni kipindupindu.
Zimbabwe imekuwa ikikabiliwa na mlipuko wa kipindupindu mara kwa mara.
Watu zaidi ya elfu nne waliripotiwa kufariki katika mlipuko wa mwaka wa 2008 na 2009 na kuambukiza wengine karibia laki moja.
Mnamo mwezi Agosti, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Unicef lilihusisha milipuko hiyo na miundombinu duni ya vyoo, mifereji ya maji taka isiyokuwa katika ubora pamoja na ukusanyaji duni wa taka, huku kukiwa na idadi ya watu mijini nchini humo ikionekana kuwa kwa kas