Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi yake ya uchochezi inayomkabili.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka kudai kuwa upande wa mashitaka umefunga ushahidi katika kesi hiyo .
Zitto ambaye anatetewa na Wakili Jebra Kambole ataanza kujitetea Machi 17 hadi 20 mwaka huu 2020 na anatarajia kuwa na mashahidi 10.
Akitoa uamuzi huo Hakimu Shaidi alisema, amepitia ushahidi wote wa mashahidi ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu, hivyo atatakiwa kujitetea.
Baada ya Hakimu kueleza hayo, Zitto alidai kuwa atajitetea kwa njia ya kiapo na anatarajia kuleta mashahidi 10 katika kesi hiyo.
Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 17,18,19 na 20 mwaka huu.
Awali Wakili wa Serikali Kweka alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya uamuzi lakini wanataka kufahamu kwa nini mshitakiwa Zitto akufika mahakamani Februari 10 mwaka huu wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya uamuzi.
Akijibu hoja hiyo, Zitto alidai kuwa alikuwa anaumwa na alitoa barua za hospitalini kudhibitisha kauli hiyo aliyohitoa.
Hata hivyo upande wa mashitaka ulidai kuwa hawaielewi barua hiyo ndipo Zitto aliwajibu kuwa waende ubalozi wa Marekani kujiridhisha.
Katika kesi ya msingi Zitto anakabiliwa na mashitaka matatu ya uchochezi ambapo, anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.
BREAKING LIVE : PIGO KWA MBOWE, MASHINJI APOKELEWA CCM