Asubuhi June 08 2016 Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameitikia wito kutoka kwa mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar es salaam. Zitto amefika kituoni hapo na ametakiwa atoe maelezo kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa June 5 2016.Baada ya kutoka Zitto ameyaeleza haya……….
>>>’nimesikitika tu kwamba sasa hivi tumefikia hali ambayo unapoenda kwenye mikutano kama kiongozi wa siasa unaanza kufikiria useme nini au usiseme nini, hali ambayo haikuwepo kwa takribani miaka 10 iliyopita tulikuwa huru kabisa kuweza kueleza mawazo yetu na hatua mbalimbali za kisiasa’.
>>>’takribani kila kitu tulichokizungumza kwenye mkutano kwa hiyo inaonyesha dhahiri kwamba ile fursa ambayo tumekuwa nayo siku zote ya kisiasa ya kuweza kujieleza na kueleza mawazo yetu inaminywa sasa, tusubiri jumatano wanasheria watakuwa wanafahamu kwamba hili jambo litakwenda mahakamani au litakuaje‘:-Zitto Kabwe
Polisi wamemruhusu Zitto kuendelea na shughuli zake baada ya kupewa dhamana na jumatano ijayo ametakiwa aripoti tena polisi na kama kutakuwa na kitu cha ziada kitaelezwa siku hiyo, hata hivyo wakili wa Zitto Kabwe hakuwa tayari kuweka wazi sehemu ya hotuba ambayo ililileta utata kwa sababu kuwa suala hili bado liko chini ya upelelezi.
ULIKOSA ALICHOONGEA ZITTO BAADA YA WANAFUNZI 700 WA UDOMKUFUKUZWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE