Hapa nanukuu sentensi za mwisho alizosema Zitto Kabwe wakati akiaga Bungeni juzi March 20 2015; “Tumeisimamia pamoja Serikali na ninajivunia kuwa sehemu ya Bunge hili la kumi.. Na Mungu akipenda tutakuwa pamoja mwezi November… Kwaherini.. Asanteni sana”– Zitto Kabwe.
Huenda kila mtu alikuwa na hamu kutaka kujua baada ya Zitto KABWE kujiuzulu Ubunge baada ya CHADEMA kumfuta uanachama, atarudi Bungeni kwa ticket ya Chama gani?
Jibu niko nalo tayari, Zitto Kabwe tayari amechukua kadi ya kujiunga Chama cha ACT kama ambavyo magazeti mengi yaliandika jana kwamba Chama hicho kilikuwa kikimsubiri muda wowote Zitto kujiunga nacho.
Kaa karibu na millardayo.com, #AMPLIFAYA.. vingi utavifahamu EXCLUSIVE kuhusu uamuzi huu wa Zitto Kabwe mtu wangu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook