Mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic ,38, Imeripotiwa kuwa ataendelea kusalia nchini kwao Sweden na kufanya mazoezi na timu ya Hammarby hadi Ligi Kuu Serie A irudi.
Zlatan alirejea kwao Sweden baada ya Ligi Kuu Italia Serie A kusimama sababu ya mlipuko wa virusi vya corona, hivyo kurejea kwake kutategemeana na kutangazwa kwa tarehe mpya kuendelea kwa msimu.
Hata hivyo hatma ya Zlatan nchini Sweden anafanya mazoezi na timu ambayo yeye ni sehemu ya wamiliki, Lockdown Italia inamalizika May 3 huku May 9 ndio itatangazwa kurejea kwa Ligi kuu na ratiba.